Friday, August 3, 2012

RATIBA YA MICHUANO YA DIMBA LA MABINGWA YA BancABC SUP8R YAZINDULIWA RASMI.



  Mkurugenzi Mtendaji wa Muunganiko wa Makampuni ya BancABC, Douglas Munatsi(kulia) akimkabidhi Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Athuman  Nyamlani kwa ajili ya mashindano ya BancABC SUP8R wakati wa uzinduzi rasmi uliofanyika Dar es Salaam.
  Uongozi wa BancABC na TFF wakiwa wameshikira Kombe kuashira Baraka njema na kutakia mashindano mema ya BancABC SUP8R .Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Hoseah,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Athuman  Nyamlani,Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Nchini,Boniphace Nyoni na Mkurugenzi Mtendaji wa Muunganiko wa Makampuni ya BancABC, Douglas Munatsi
  Picha ya Pamoja ya Uongozi wa BancABC,Mabalozi wa BancABC kutoka Kampuni ya Integreted Comminications na Kombe.
Picha ya Pamoja ya Mabalozi wa BancABC kutoka Integrated Comminications

RATIBA YA MICHUANO YA“BancABC SUP8R 2012” YATANGAZWA!.

Draw maalumyakupangaratibakamiliyamichuanoya“BancABC SUP8R 2012”imechezeshwaleohiijijini Dar Es Salaam, zoezihilililitanguliwanakutajwakwamajinayatimunaneambazoJumamosihiizitaingiaviwanjanikatikamikoaya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanzana Zanzibar.
Akizingumzanawaandishiwahabari, afisahabariwa TFF bwana Boniface Wamburaalisemamashindanohayayatashirikishatimutatuzilizofanyavizurikwenyeligikuuya Tanzania barailiyoishayaani Simba, YanganaAzamzikiungananatimumpyailiyofaulukuingialigikuuyabaramsimuujaoyaaniMgambo JKT kutokaHandeni. Timuhizinnezitaungananatimuzinazoshirikikutoka Zanzibar ambazozilifanyavizurikwenyemsimuwaligikuuya Zanzibar uliomalizika. TimuhiziniJamhuri, Zima Motona Super Falconambazozitaungananatimuiliyofaulukuingialigikuuya Zanzibar msimuujaoyaanitimuyaMtende Rangers.
SikuyaJumamosimechizaufunguzizitachezwakwawakatimmojakatikaviwanjavyotevinnevyamashindanohaya. Jijini Dar Es Salaam mechizitachezwakatikauwanjawaChamazikuleMbagala, mjiniArushakatikauwanjawaShaikhAmriAbeid, kuleMwanzakatikauwanjawa CCM Kirumbana Zanzibar katikauwanjawaAmani. Mechizotezitaanzasaakumijioni.
Naye Bwana BoniNyoni, mkurugenzimtendajiwaBancABCalisemabenkihiiimedhaminimashindanohayakwalengo la kuwazawadiawateja wake kwakuwapaburudanihiiyampirawamiguu. Alisemahiinikutimizapiatamko la serikalikwamakampuninataasisibinafsikujihusishanamichezo. Alisemajumlayaudhaminiwamichuanoya“BancABC SUP8R 2012”nishilingimilionimiananethemanini (880,000,000/=) ambazozinajumuisha;
§  Gharamazamatayarishonauratibuwamichuano.
§  Malazikwatimunaviongozi.
§  Usafiriwatimu, wandegenaulewavituoni.
Zawadizamichuanoya“BancABC SUP8R 2012” nikamaifuatavyo;
§  Timuitakayoibukamshindiitazoakitita chashilingimilioni 40 taslimu.
§  Mshindiwapiliitajinyakuliashilingimilioni 20.
§  Timu 2 zitakazotolewanusufainalizitajipatiamilioni 15 kilamoja.
§  Timu4zitakazotolewarobofainalizitajipatiamilioni5 kilamoja.
§  Mchezaji bora wamashindanoatanyakuamilioni 2 nalaki 5 na
§  Mfungaji bora wamashindanoatanyakuamilioni 2 taslimu.
Bwana Nyonialiwaombawatanzaniakujitokezakwawingikushangiliatimuzaonakushuhudiakiwango bora cha kandandakutokakwatimuhizizilizoshikanafasizajuukwenyeligiziliyokwisha Tanzania Bara navisiwani. Mashindanohayayatazipatimuhizinafasiyakujaribuvikosivyaovipyavinavyounganishawachezajiwapyawaliosajiliwana wale walioposasa. Inatoanafasipiakwatimuzinazoingialigikuukuwaonyeshawashabikiwasokakwambakwelizikotayarikukabilimikikimikikiyaligikuuitakapoanzahivikaribuni.

Bwana BonialimalizakwakuwaombawashabikiwasokakutembeleamatawiyaBancABCyaliyokoKariakoo, Quality Centre, Upanganamtaawa Swahili kuleArushailikujipatiahuduma bora zabenkihii.
Naye Bwana Douglas T Munatsi, MurugenzimtendajiwamuunganikowamakampuniyaBancABCalisemakwa wale ambaohawafahamu, BancABCilianzishamichuanoyamtoanowatimunanekwamaraya kwanza nchini Zimbabwe mwaka 2008. Michuanohiiambayokwasasainajulikanakama“BancABC SUP8R” ilikuwananiayakufanyikamaramojatuilikutangazakuingiakwaBancABCkatikasektayahudumazakibenki. Lakinikutokananamafanikiomakubwayaliyopatikanakatikamiakamitatu,wakaamuamichuanoya“BancABC SUP8R”ifanyikekilamwakailikuwapanafasikujumuikanawashabikiwakweliwa“BancABC SUP8R”viwanjani. HiinifursapiayafurahakwamamilioniyawapendasokakatikamaeneombalimbaliyaAfrika.
Bwana MunatsialiendeleakusemakwambaBancABCinajitahidisanakuwakinarakatikahudumazakibenkinapiakuongozakatikaubunifu. NiayamuunganikowamakampuniyaBancABCimekuwakuhakikishakwambamafanikioyaudhaminiwamichuanoya“BancABC SUP8R”yanafikapiakatikanchizoteambazoBancABCinatoahudumazakibenki. Mipangoyamudamrefunikuhakikishawashindiwa“BancABC SUP8R”wakilanchiwanakutanishwailikupatamshindimmojawanchizote. Alimalizakwakusema, “Ni kwaheshimakubwanafurahatelenazinduarasmimichuanoya“BancABC SUP8R” hapa Tanzania nanawashukurusana TFF kwakukubalikuungananaBancABC”.
Fainalizamashindanohayazinatarajiwakufanyikakatikauwanjampyawataifahapa Dar EsSalaasikuJumamosiyatarehe 18 mwezihuu.

Saturday, July 28, 2012

DVD ZA SUPER D BOXING COACH ZILIZOPO SOKONI


DVD ZA SUPER D BOXING COACH ZILIZOPO SOKONI
DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI ZIPO MTAANI KWA AJILI YA MAFUNZO YA MCHEZO HUO HIVI SASA KWA MATAJI YA JUMLA NA REJAREJA PIGA SIMU 0787/0774/0715/0754/0733/0713-406938 AU FIKA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI 0652755838

Sunday, February 26, 2012

TPBC kuingia mkataba na Jiji la Arusha

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imeanza mazungumzo ya awali ya kuingia kwenye mkataba wa miaka mitano na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kikao cha kwanza cha makubaliano haya kilifanyika tarehe February 16, 2012 jijini Arusha ambapo suala zima la Utalii wa Michezo (Sports Tourism) lilitawala.
Katika mazungumzo hayo, Jiji la Arusha liliwakilishwa na Mstahiki Meya Gaudence Lyimo na Naibu Meya Sakeyan. Kwa upande wa TPBC, IBF na CBC waliwakilishwa na Rais wake Onesmo Ngowi pamoja na Kamishna wa TPBC mkoa Arusha Roman Chuwa ambaye ni mfanyabishara wa utalii anayemiliki kampuni ya Equatorial Safaris and Tours ya jijini Arusha.
Makubaliano haya ambayo yanarajia kuzaa mkataba wa miaka mitano kati ya wabia hawa (Halmashauri ya Jiji la Arusha na TPBC) yanalenga kujenga ajira kwa vijana, kutangaza jiji la Arusha kama kitovu cha utalii wa ndani na nje (Destination Market), kujenga biashara za nje (Foreign trades) pamoja na kuanzisha na kuendeleza mtandao vituo (Sports gyms) vya mafunzo ya kuibua vipaji vya michezo kwa vijana katika kata zote za Jiji la Arusha.
Katika makubaliano haya, Ngowi anawakilisha pia Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lililo na makao makuu yake makuu jijini New Jersey, nchini Marekani ambalo litatumika kutangaza jiji la Arusha kama kitovu cha biashara ya kitalii kwa wananchi wa Marekani na nchi zote za Amerika ya Kaskazini, Kusini ya Caribbean.

IBF ina mtandao katika nchi zaidi ya 78 na itasaidia sana kutangaza jiji la Arusha kwenye mtanado wake.

Mkataba huo pia unajumuisha Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola Commonwealth Boxing Council (CBC) ambalo Onesmo Ngowi ni Mkurugenzi wa Bodi yake. CBC litatoa vibali vya mapambano ya kugombea ubingwa wa Jumuiya ya Madola.

Aidha, makubaliano haya yatalipatia jiji la Arusha mapambano manne (4) ya kimataifa kwa mwaka yatayosimamiwa na IBF ambayo yatarushwa na luninga kwenye nchi zaidi ya 78 duniani zikiweko Marekani, nchi za Ulaya, Japan na Australia ambazo ndio chemecheem kubwa ay watalii Tanzania.

Imetolewa na

Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
Director, Commonwealth (British Empire) Boxing Council (CBC)
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)

Tuesday, February 21, 2012

Mwenyekiti Wazazi (CCM) Tanga ajiunga Chadema

Na Peter Mwenda,Tanga

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa Kata ya Maramo ya Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Muheza mjini na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Bw. Hassan Mrisho Mngazija amejiondoa chama hicho na kujiunga na Chadema.
Bw. Mngazija ni mmoja wa wanachama wapya zaidi ya 500 walikabidhiwa kadi mpya za kujiunga na Chadema katika mikutano ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara Bw. Zitto Kabwe katika mkoa wa Tanga.

"Akihutubia mikutano ya hadhara katika Wilaya ya Muheza, akiwa kwenye ziara ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga Bw. Zitto Kabwe alisema kuwa hali ya wananchi kukosa matumaini kwa watawala wao (CCM) ni moja ya dalili mbaya kwa utawala wowote ule na tishio kubwa la amani ya nchi.
Alisema iwapo hali ya wananchi kukosa matumaini inayojionesha miongoni mwa Watanzania kutokana na utawala mbovu usiojali matatizo yanayowakabili na kuacha hali hiyo iendelee bila kutafutiwa suluhisho, itakuwa ni hatari kwa watawala na mstakabali wa nchi.

Bw. Zitto alisema tabia ya viongozi kutowasemea wananchi wanyonge, hasa wale wa vijijini, chama hicho kimejitolea kuifanya kazi hiyo katika majukwaa mbalimbali, ikiwemo mikutano ya hadhara, bungeni na kokote kule, ambako kitaweza kupaza sauti kuonesha uongozi mbadala namna ambavyo nchi inapaswa kuongozwa, kikijikita kutoa suluhisho ya matatizo hayo.

“Wananchi mmepoteza matumaini, mmekata tamaa, hamuwaamini tena watawala walioko madarakani, mmepoteza matumaini na CCM. Kwa mambo mliyofanyiwa miaka nenda rudi na chama hicho, hamtuamini tena wanasiasa, kila anayekuja mnamuona ni yule yule, Kila mkitusikiliza mnatusikia tunazozana kuhusu posho, tunagombania maslahi yetu, badala ya kuwasemea ninyi wanyonge wenye nchi"alisema Bw. Zitto na kushangiliwa na umati wa wananchi walijitokeza kumsikiliza.
Alisema kati ya mambo ambayo yataipasua nchi hii ni suala la ukosefu wa ajira kwa vijana na ufisadi, rushwa na ubadhirifu upande mwingine.
Alisema miaka mitano sasa wananchi wamekuwa wakisoma katika magazeti na kusikia fulani kapiga pale, fulani kapiga hapa, mkurugenzi yule wa halmashauri kaiba pale, mkurugenzi huyu wa shirika la umma kaiba hapa na mengine ya wanasiasa mafisadi wanazidi kupoteza matumaini.

Bw. Zitto alisema matukio hayo yanawalea vibaya watoto  wa kitanzania Wataamini kuwa ukitaka kuishi katika nchi hii ni lazima uwe fisadi, kitu ambacho sikweli. Watawala sasa wanafikiria kula tu, wanafikiria maslahi yao, hawasemei tena wananchi maskini, hasa walioko vijijini. Tangu alipofariki Mwalimu Nyerere, aliyekuwa watetezi wa wanyonge, wananchi wa vijijini wamekosa msemaji kabisa,” alisema Zitto.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alitolea mfano wa namna wananchi wa vijijini walivyotelekezwa, akisema kuwa kila inapotokea umeme umekatika maeneo ya miji mikubwa, nchi husemwa ‘iko gizani’, bila kujali kuwa kuna wananchi tangu Tanzania ipate uhuru ‘wako gizani’ miaka yote, lakini athari za kukosekana kwa nishati hiyo ikiendelea kuwaathiri.

Mbali ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, Zitto pia anafanya ziara mkoani Tanga, kwa ajili ya kuifafanua hoja yake juu ya zao la mkonge, aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano wa bunge uliopita.
mwisho