Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imeanza mazungumzo ya awali ya kuingia kwenye mkataba wa miaka mitano na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kikao cha kwanza cha makubaliano haya kilifanyika tarehe February 16, 2012 jijini Arusha ambapo suala zima la Utalii wa Michezo (Sports Tourism) lilitawala.
Katika mazungumzo hayo, Jiji la Arusha liliwakilishwa na Mstahiki Meya Gaudence Lyimo na Naibu Meya Sakeyan. Kwa upande wa TPBC, IBF na CBC waliwakilishwa na Rais wake Onesmo Ngowi pamoja na Kamishna wa TPBC mkoa Arusha Roman Chuwa ambaye ni mfanyabishara wa utalii anayemiliki kampuni ya Equatorial Safaris and Tours ya jijini Arusha.
Makubaliano haya ambayo yanarajia kuzaa mkataba wa miaka mitano kati ya wabia hawa (Halmashauri ya Jiji la Arusha na TPBC) yanalenga kujenga ajira kwa vijana, kutangaza jiji la Arusha kama kitovu cha utalii wa ndani na nje (Destination Market), kujenga biashara za nje (Foreign trades) pamoja na kuanzisha na kuendeleza mtandao vituo (Sports gyms) vya mafunzo ya kuibua vipaji vya michezo kwa vijana katika kata zote za Jiji la Arusha.
Katika makubaliano haya, Ngowi anawakilisha pia Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lililo na makao makuu yake makuu jijini New Jersey, nchini Marekani ambalo litatumika kutangaza jiji la Arusha kama kitovu cha biashara ya kitalii kwa wananchi wa Marekani na nchi zote za Amerika ya Kaskazini, Kusini ya Caribbean.
IBF ina mtandao katika nchi zaidi ya 78 na itasaidia sana kutangaza jiji la Arusha kwenye mtanado wake.
Mkataba huo pia unajumuisha Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola Commonwealth Boxing Council (CBC) ambalo Onesmo Ngowi ni Mkurugenzi wa Bodi yake. CBC litatoa vibali vya mapambano ya kugombea ubingwa wa Jumuiya ya Madola.
Aidha, makubaliano haya yatalipatia jiji la Arusha mapambano manne (4) ya kimataifa kwa mwaka yatayosimamiwa na IBF ambayo yatarushwa na luninga kwenye nchi zaidi ya 78 duniani zikiweko Marekani, nchi za Ulaya, Japan na Australia ambazo ndio chemecheem kubwa ay watalii Tanzania.
Imetolewa na
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
Director, Commonwealth (British Empire) Boxing Council (CBC)
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Sunday, February 26, 2012
Tuesday, February 21, 2012
Mwenyekiti Wazazi (CCM) Tanga ajiunga Chadema
Na Peter Mwenda,Tanga
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa Kata ya Maramo ya Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Muheza mjini na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Bw. Hassan Mrisho Mngazija amejiondoa chama hicho na kujiunga na Chadema.
Bw. Mngazija ni mmoja wa wanachama wapya zaidi ya 500 walikabidhiwa kadi mpya za kujiunga na Chadema katika mikutano ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara Bw. Zitto Kabwe katika mkoa wa Tanga.
"Akihutubia mikutano ya hadhara katika Wilaya ya Muheza, akiwa kwenye ziara ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga Bw. Zitto Kabwe alisema kuwa hali ya wananchi kukosa matumaini kwa watawala wao (CCM) ni moja ya dalili mbaya kwa utawala wowote ule na tishio kubwa la amani ya nchi.
Alisema iwapo hali ya wananchi kukosa matumaini inayojionesha miongoni mwa Watanzania kutokana na utawala mbovu usiojali matatizo yanayowakabili na kuacha hali hiyo iendelee bila kutafutiwa suluhisho, itakuwa ni hatari kwa watawala na mstakabali wa nchi.
Bw. Zitto alisema tabia ya viongozi kutowasemea wananchi wanyonge, hasa wale wa vijijini, chama hicho kimejitolea kuifanya kazi hiyo katika majukwaa mbalimbali, ikiwemo mikutano ya hadhara, bungeni na kokote kule, ambako kitaweza kupaza sauti kuonesha uongozi mbadala namna ambavyo nchi inapaswa kuongozwa, kikijikita kutoa suluhisho ya matatizo hayo.
“Wananchi mmepoteza matumaini, mmekata tamaa, hamuwaamini tena watawala walioko madarakani, mmepoteza matumaini na CCM. Kwa mambo mliyofanyiwa miaka nenda rudi na chama hicho, hamtuamini tena wanasiasa, kila anayekuja mnamuona ni yule yule, Kila mkitusikiliza mnatusikia tunazozana kuhusu posho, tunagombania maslahi yetu, badala ya kuwasemea ninyi wanyonge wenye nchi"alisema Bw. Zitto na kushangiliwa na umati wa wananchi walijitokeza kumsikiliza.
Alisema kati ya mambo ambayo yataipasua nchi hii ni suala la ukosefu wa ajira kwa vijana na ufisadi, rushwa na ubadhirifu upande mwingine.
Alisema miaka mitano sasa wananchi wamekuwa wakisoma katika magazeti na kusikia fulani kapiga pale, fulani kapiga hapa, mkurugenzi yule wa halmashauri kaiba pale, mkurugenzi huyu wa shirika la umma kaiba hapa na mengine ya wanasiasa mafisadi wanazidi kupoteza matumaini.
Bw. Zitto alisema matukio hayo yanawalea vibaya watoto wa kitanzania Wataamini kuwa ukitaka kuishi katika nchi hii ni lazima uwe fisadi, kitu ambacho sikweli. Watawala sasa wanafikiria kula tu, wanafikiria maslahi yao, hawasemei tena wananchi maskini, hasa walioko vijijini. Tangu alipofariki Mwalimu Nyerere, aliyekuwa watetezi wa wanyonge, wananchi wa vijijini wamekosa msemaji kabisa,” alisema Zitto.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alitolea mfano wa namna wananchi wa vijijini walivyotelekezwa, akisema kuwa kila inapotokea umeme umekatika maeneo ya miji mikubwa, nchi husemwa ‘iko gizani’, bila kujali kuwa kuna wananchi tangu Tanzania ipate uhuru ‘wako gizani’ miaka yote, lakini athari za kukosekana kwa nishati hiyo ikiendelea kuwaathiri.
Mbali ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, Zitto pia anafanya ziara mkoani Tanga, kwa ajili ya kuifafanua hoja yake juu ya zao la mkonge, aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano wa bunge uliopita.
mwisho

Subscribe to:
Posts (Atom)